Kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula ameitaka serikali kuweka mikakati maalum ya kusaidia uchumi wa sekta ya juakali na kilimo msimu huu wa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.
Wetangula amesema ipo haja ya serikali kuwapa wakulima pembejeo na usaidizi zaidi ili kuwezesha taifa kujitegemea kilimo ikizingatiwa mataifa mengi yanayotegemewa kuzalisha vyakula yameadhirika.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, seneta huyo wa Bungoma licha ya kusifia uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta hapo jana, ametoa changamoto kwa serikali kupiga jeki sekta ya juakali inayotoa ajira kwa idadi kubwa kwa wakenya mbali na kuitaka serikali kuwapa wakenya vyakula iwapo taifa litasitisha shughuli zote za lockdown Vile vile amelitaka Bunge lirejelee vikao ili kuangazia maswala muhimu kuhusu janga la korona.