Acheni Siasa Katika Vita Dhidi ya Ufisadi

Aliyekuwa Inspekta Jenerali wa polisi David Kimaiyo amewasuta baadhi ya viongozi nchini kwa kile amesema kuingiza siasa katika kesi ya kashfa inayomkabili aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa.

Akiongea na kituo hiki kwa njia ya simu, Kimaiyo, amesema viongozi hao wanapaswa kuipa nafasi tume ya maadili na kupambana na ufisadi -EACC na idara ya upelelezi -DCI kufanya uchunguzi wao pasi na kuingizwa siasa. Hata hivyo, amesisitiza kuwa iwapo wanasiasa wataendelea kuhusisha siasa  kwenye masuala muhimu, basi ni wazi kuwa hata wao hawako tayari kupiga vita ufisadi humu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *