Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya kupambamba na ukeketaji wa wanawake hii leo serikali itaendelea kukaza kamba katika vita dhidi ya ukeketaji.
Naibu rais William ruto amesema wadau wote wanafaa kushirikiana katika makabiliano hayo ili kuhakikisha visa vya ukeketaji vimepungua.Wakati sherehe hizi zikipangwa kufanyika katika kaunti ya isiolo wizara ya jinsia na utumishi wa umma shirika la umoja wa mataifa kuhusu idadi ya watu na mandiya watu ambao kaunti 22 zinakabiliwa na ukeketaji walikongamana katika kaunti ya isiolo hapo jana ili kuanzisha kampeni za kuzuia ukeketaji na kumalizia kabisa kufikia mwisho wa mwaka wa 2020 kama raisi Kenyatta alivyoagiza. Rachel shebesh waziri msimamizi katika wizara ya jinsia amesema kuwavumilia wanaoedesha ukeketaji kumefika mwisho na watakaopatikana watakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria.