Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wikendi hii.
Haya ni kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini ambayo imesema kuwa mvua kubwa itashuhudiwa katika maeneo ya Migori, Siaya, Homabay, Kisumu, Nyamira, Kericho, Bomet, Nakuru, Kiambu, Nyandarua, Nyeri pamoja na Muranga
Maeneo mengine ni pamoja na Meru, Kirinyaga, Tharaka Nithi, Kitui, Machakos, Makueni, Tana River, Garissa, Wajir, Isiolo, Samburu, Marsabit na Turkana. Aidha idara hiyo imewataka wananchi kuchukua tahadhari ya mapema hususan maeneo ambayo huenda yakashuhudia mafuriko.