Takriban walimu elfu mia moja wanatarajiwa kupata mafunzo kuhusu mtaala mpya wa u milisi (CBC) elimu kuanzia hii leo.
Afisa mnkuu mtendaji wa tume ya huduma za walimu TSC Nancy Macharia amesema kwamba wanaolengwa ni wakuu wa shule na walimu wanaotoa mafunzo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Aidha Macharia amesema walimu wawili wa gredi ya nne, kwanza na pili hasa wanaofunza hisabati watashirikishwa kwenye mpango huo utakaogharimu shilingi billion moja.
Kwa mujibu wa TSC, mafunzo hayo yanalenga kuwapa walimu maandalizi kwa ajili ya kurejelewa kikamilifu kwa masomo kuanzia Januari mwakani.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa njia ya video na yanatarajiwa kukamilika Desemba 22, mwaka huu. Ikumbukwe kuwa mwaka jana walimu wapatao 400,000 walipokea mafunzo kuhusu CBC kwenye mpango uliogharibu shilingi milioni 400.