Huenda Kenya kukashihudiwa idadi ndogo ya Watalii Mwaka huu

Wamerakani wametahadharishwa dhidi ya kuja nchini Kenya kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa corona.

Kituo cha kuthibiti maradhi nchini humo CDC kimeipa Kenya kiwango cha nne za tahadhari ya hatari hatua inayomaanisha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mtu kuambukizwa virusi hivyo nchini.

Hii ni licha ya nchi hiyo kusajili Zaidi ya visa laki mbili kufikia siku ya jumatano ikilinganishwa na visa 85,000 nchini Kenya. Kupitia ilani hiyo ya CDC wamerekani wameonya dhidi ya kufanya ziara za kuja nchini.

Ilani hiyo imesema kabla ya wamerakani kusafiri wanafaa kupimwa kwanza kati ya siku moja hadi tatu kabla ya kusafiri. Kenya ni miongoni mwa mataifa mengine ya Afrika mashariki zikiwemo Uganda, Tanzania na Burundi ambazo zimepewa ilani ya kiwango cha 4 na Marekani. Rwanda ina kiwango cha 1 hatua inayomanisha kwamba uwezekano wa mtu kuambukizwa ugonjwa huo uko chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *