Wito umetolewa kwa rais Uhuru Kenyatta kuangazia ufufuzi wa uchumi wa chi wakati wa hotuba yake kwa bunge la taifa na la seneti.
Haya ni kwa mujibu wa baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Uasin Gishu ambao wanadai kuathirika pakubwa sana kiuchumi kutokana na janga la Corona.
Wamesema kuwa ingekuwa bora rais kugusia swala hili kwa undani na jinsi gani uchumi utafufuka ili maisha ya wananchi yawe sawa kwa vile wengi wanapitia hali ngumu ya kupata pato la kila siku. Wamemtaka rais pia kuangazia sekta ya afya kwa kuwahakikishia uhalali wa chanjo ya covid-19 ambayo imedhibitishwa na watafiti kuwa ni salama kwa matumizi huku wakimtaka kuweka mikakati zaidi ya kupambana na janga hili.