Shughuli katika kituo cha damu mjini eldoret zimetatizika kufuatia mgomo wa wahudumu wa afya kituoni humo .
Wahudumu hao wamesema tangu kugatuliwa sekta ya afya hawajawahi pandishwa vyeo licha ya wengi wao kuongeza masomo. Kando na hayo mazingira wanayofanyia kazi siyo ya kuridhisha kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona.