Khwisero – Mwanamake anyimwa Urithi kwa kukosa Kupata mtoto

Mwanamke mmoja kutoka kijiji cha Khwisero amefurushwa  na mashemejiye ili kumzuia  kurithi chochote kwenye boma hilo baada ya kukosa kufanikiwa kupata mtoto katika ndoa baada ya mumewe kufariki.

Millicent Aoko alikuwa amepewa notisi ya  kuhama licha ya kuishi na mumewe zaidi ya miaka kumi iliyopita. Anadai licha ya chifu kujaribu kutatua mgogoro uliokuwa kati yao  mashemejiye walifika na kubomoa nyumba yake huku wakibeba baadhi ya mali alioachiwa na mumewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *