Cheptobot, Marakwet – Jirani amuuwa Jirani mwenzake

Maafisa wa polisi wamemtia mbaroni mwanamume mmoja anayeshukiwa kumuuwa jirani wake katika kjiji cha Cheptobot eneo bunge la Marakwet Magharibi , Kaunti ya Elgeyo Mrakwet.

Polisi wanasema walifanikiwa kumpata jamaa huyo kwa jina Evans Kipchirchir baada ya kutoroka   kifuatia kifo cha jirani wake 

Mkuu wa polisi  katika eneo hilo John Matasi amesema bado wanawasaka washukiwa wengine  tano ambao  walishirikiana kumuua jirani wao kufuatia mzozo wa ardhi. Matasi aidha ameongeza kuwa washukiwa wengine wanaaminika kutorokea Kaunti ndogo ya Marakwet mashariki, huku akiwataka walio na ripoti kuhusiana na kisa hicho kuripoti kwa ofisi husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *