Wakristo wametakiwa kuwa karibu na wenye changamoto tofauti katika maisha ili kuendeleza safari ya imani yao.
Kwenye homilia katika kanisa la moyo mtakatifu wa yesu Kathedrali Eldoret, padre David Kiptoo amewahimiza wakristo kutojitenga na walio na changamoto haswa za magonjwa na wale wasio mtambua mungu katika kuwasaidia kupata mwelekeo bora.
Ametaja sala kama silaha muhimu kwa maisha ya mwanadamu kwa kupambana na hali ngumu kila mtu anapitia kwa kuwa karibu na mungu na pia kubadilisha mienendo ya asiyetambua kristo.
amesema kuwa kama mkristo ni vyema kumpatanisha yule asiyekuwa na Kristo pamoja na mungu katika imani na sala za kila siku.
aidha kujenga imani ya mwingine ndio njia pekee ya kukombolewa katika kristo na kujitakia baraka za milele maishani.
