Serikali kupitia mradi wa ushanga initiative inalenga kuwapa mafunzo kina mama kutoka jamii za wafugaji kuhusu jinsi ya kutumia shanga kutengeneza bidhaa zitakazowapa pesa ili kuwasaidia kujikimu.
Mradi huo unalenga kutoa mafunzo kwa akina mama kutoka kaunti saba ikiwemo pokoti magharibi huku akina mama 150 wakisajiliwa kutoka kwa kila kaunti ndogo.
Katibu katika wizara ya michezo na utamaduni Josphedha Mukhobe anasema kuwa mradi huo unalenga kuwawezesha kina mama kujitegemea kupitia njia ya kitamaduni ikiwemo kutengeneza bidhaa kupitia shanga.
Gavana wa kaunti hiyo john lonyangapuo amesifia hatua hiyo kama njia mwafaka ya kuimarisha uchumi eneo hilo na kuwainua kina mama.