kaunti ya transnzoia imerekodi zaidi ya visa vya mimba za mapema elfu 11 huku wito ukitolewa kwa washikadu wote kushirikiana katika kukabili visa hivi.
akitoa takwimu hizo naibu kamishina wa kaunti hiyo evans kauma amesema kuwa visa hivi vimeongezeka miongoni mwa vijana wa miaka 14 kaunti ndogo ya endebes ikiongoza kwa visa hivyo nayo ya kiminini ikiongoza kati ya miaka 14 na 19.
naye waziri wa afya kaunti hii clare wanyama wamewataka washikadau wote kushirikiana katika kumaliza jinamizi hili.