Aliyekuwa spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amedai kwamba maisha yake yalikuwa hatarini akiwa jumba la City Hall kabla ya kuchukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake.
Akisimulia masaibu yake siku ya Jumatano katika mahojiana na runinga mmoja humu nchini, Elachi alisema kwamba kuna watu waliokuwa wameleta tindi kali aina ya ( sulfuric acid) katika bunge hilo la kaunti kwa lengo la kumuumiza.
Elachi alijiuzulu siku ya Jumanne asubuhi, na kusema kwamba alikuwa anaingia katika awamu nyingine ya taaluma yake ya kisiasa na kurejea katika eneo bunge la Dagoret North.
Alisema kwamba City Hall inamaswala mengi ambayo hayajatatuliwa ukiwemo usimamizi wa vyoo vya kaunti na kwamba baadhi ya watu katika bunge hilo wamevutiwa. Spika huyo wa zamani pia alisema kwamba, mkurugenzi wa bodi simamizi ya jiji la Nairobi Mohamed Badi pia atakumbana na matatizo.
