KNUT yasema Shule hazifai kufunguliwa kwa sasa.

Chama cha walimu nchini KNUT kimeonya kuwa huenda kukawa na athari kubwa, iwapo shule zitafunguliwa mwezi ujao.

Katibu mkuu Wilson Sossion anasema mpango huo wa kufungua shule haufai kwa sasa na unapaswa kutathminiwa kwa makini sana. Waziri wa elimu George Magoha aliteuwa jopokazi la wanachama 9 kuunda mchakato wa kurejelewa kwa shughuli za masomo.

Tukisalia maneno ya elimu, hivi karibuni wazazi watapokea mwongozo wa jinsi ya kuwasaidia wanao wanaposoma nyumbani. Katibu msimamizi wa elimu Mumina Bonaya anasema hii ni kwa sababu wamepokea ripoti kuwa wazazi wanasumbuka kuhakikisha wanao wanaendelea masomo wakiwa nyumbani baada ya shule kufungwa kutokana na janga hili la Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *