Walimu wakuu wataka mitihani ya kitaifa kuahirishwa

Walimu wakuu wanataka mitihani ya kitaifa kuahirishwa wakisema kwamba ongezeko la maambukizi ya coronavirus  huenda likachelewesha kufunguliwa kwa shule.

Serikali ilizifunga shule zote mwezi machi kwa sababu ya janga la coronavirus na tathminmi ya wizara ya afya kwamba huenda virusi hivyo vikafika kilele chake mwezi agosti inamaanisha kwamba muhula wote utakuwa umekwisha bila wanafunzi kurejea shuleni.

Kalenda ya baraza la mtihani nchini KNEC inaonyesha kwamba mtihani wa KCPE utaanza oktoba tarehe 27 ilhali ule wa KCSE utaanza Novemba tarehe 2.

Rais Uhuru Kenyatta na waziri wa Elimu George Magoha wamesema kwamba kalenda ya mtihani kwa watahiniwa wote milioni 1.8  itasalia jinsi ilivyopangwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *