Hatimaye jimbo katoliki la eldoret limepata mchungaji baada ya kusimikwa kwa askofu Dominic Kimengich hii leo.
hafla ya hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini ilianza rasmi na misa ambayo iliongozwa kwa sala fupi kutoka kwa mwadhama kadinali Yohane Njue kabla ya askofu Dominic kimengich Kubusu msalaba, kukariri kanuni ya imani, na kuketishwa katika kiti chake rasmi almaarifu kathedra.
Kwenye homilia iliyotolewa na askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu askofu Philip Anyolo, aliwataka wakristu kushirikiana na askofu huyo mpya ili kufanikisha shughuli za kueneza injili Kote Jimboni, akisema hii ilikuwa kilio ambacho kiligeuzwa kuwa furaha baada ya jimbo hili miaka miwili iliyopita kumpoteza askofu Cornelius Arap Korir.
Hafla hii ya kusimikwa kwa askofu Dominic Kimengich ilihudhuriwa na mwadhama kadinali Yohane Njue,mwakilishi wa Baba mtakatifu humu nchini Mathews Herbatus Van Megen askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu askofu Philip Anyolo maaskofu wa majimbo mbalimbali pamoja na maaskofu wastaafu.