Takwimu za hivi punde kuhusiana na idadi ya watu walioathirika na virusi vya Corona nchini imefikia watu 216.
Hii ni baada ya katibu katika wizara ya afya Mercy Mwangangi, kusema kuwa watu 694 wamefanyiwa vipimo vya afya na kati ya watu hao 8 walipatikana na virusi hivyo kufikisha idadi ya wale walioathirika kuwa 216.
Wakati uo huo Mwangangi amesema mtu mmoja ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha idadi ya watu walioathirika kuwa 41. Vile vile Katibu huyo amesema serikali itaanza kusambaza vifaa vya kuanza kupima watu takriban 12,000 katika kaunti zilizoathirika ikiwemo Nairobi, Mandera, Mombasa, Siaya.
Watu hao 8, 6 ni kutoka kaunti ya Nairobi, 1 kutoka Siaya na 1 Kutoka kaunti ya Nakuru.
Mwangangi aliwataka Wakenya kuendelea kujikinga na maambukizi akisema vita dhidi ya janga la ugonjwa huo vitafaulu iwapo kutakuwa na ushirikiano. Aidha alisema wizara inashirikiana na kampuni za kidijitali ili kuhakikisha kuwa Wakenya wanatumia teknolojia kupambana na covid-19. Katibu huyo pia alionya kuhusu ongezeko la mizozo ya kindoa wakati huu ambapo wengi wanazidi kuwa manyumbani