Mwandishi mashuhuri wa riwaya na mwanahabari , Profesa Walibora ameaga dunia akiwa na miaka 56.
Msomi huyo wa fasihi na mwandishi wa kitabu cha siku njema aliripotiwa kupotea ijumaa iliyopita baada ya kugongwa na gari kwenye barabara ya landhies jijini Nairobi.
Mwili wake umepatikana mapema leo katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali kuu ya Kenyatta.