Waziri wa elimu George Magoha amesema kwamba hajui lini shule na taasisi zingine za elimu zitafunguliwa.
Amesema uamuzi huo utaafikiwa wakati janga la corona litakapokuwa limedhibitiwa. Emesisitiza kuwa Maisha ya wanafunzi yana umuhimu zaidi kuliko jambo lolote lile.
Hata hivyo waziri Magoha amewahakikishia wazazi kuwa kufikia sasa ratiba ya elimu mwaka huu haijavurugwa sana kama inavyokisiwa.
Amesema kufikia sasa wanafunzi wamepoteza wiki tatu pekee za masomo katika mhula wa kwanza.
Amesema kwa sasa wanafunzi wamo kwenye likizo ya mwezi Aprili na kuondoa hofu kwamba mitihani ya kitaifa itaahirishwa.
Amesema wanafunzi wanaendelea na mafunzo kwenye mitandao na vyombo vya habari. Waziri vile vile amesema kwamba wanaweka mikakati ili kuhakikisha kwamba wanafunzi ambao hawana mitandao pia wanapata mafunzo wakati huu
Waziri ametangaza kwamba wanaendelea na mikakati mbali mbali kuhakikisha kuwa ratiba ya elimu inaendelea. Amesema watafanya uamuzi mwafaka wakati ufaao kulingana na hali itakavyokuwa kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona.