Vikao vya Bunge Vyarejelewa baada ya Kuathirika na Corona

Wabunge 198 wamejisajili kuhudhuria vikao maaluma vya leo baada ya shughuli za bunge kusitishwa kwa muda kutokana na virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa  karani wa bunge Michael Sialai, ni wabunge 53 pekee watakaoruhusiwa kuingia katika chumba cha mijadala huku wengine wakitengewa nafasi maeneo mengine katika majengo ya bunge.

 Wakati uo huo wabunge wenye matatizo ya kiafya au wakongwe  wakiombwa kutohudhuriwa.

Wabunge hao waanatarajiwa kujadili na kuidhinisha hoja kadhaa ya muhimu kabisa ikiwa ni kupiga msasa mapendekezo ya rais Uhuru Kenyatta kupunguza na kuondoa kodi mbalimbali kuwanusuru wakenya kutokana na hali ngumu ya kiuchumi. Wabunge hao pia watajadili mikakati iliyowekwa ili kukabili maambukizi ya virusi vya Corona

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *