Wekeni kiwango cha nafaka

Wakulima wa nafaka kaunti ya Uasin Gishu wameshauriwa kuweka wazi kiwango cha nafaka walicho nacho ili kuiwezesha serikali kuinunua wakati huu ambapo serikali imewataka wakenya kusalia nyumbani kutokana na janga la virusi vya Corona. Waziri wa kilimo Samuel Yego amewashauri wakazi kufika katika afisi za kilimo katika wadi zao na kupeana maelezo kuhusu kiwango cha nafaka hasa mahindi, ngano maharagwe ili kununuliwa na serikali.

Ikumbukwe kuwa wakulima wa mahindi wamekuwa wakilalamikia hatua ya bodi ya kitaifa ya mazao na nafaka- NCPB kukosa kuyanunua mazao yao mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *