Katibu mkuu katika Wizara ya Elimu, Julius Bitok, amesema kuwa wanafunzi 14 wamepoteza maisha yao kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi uliotokea katika eneo la Chesongoch, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Bitok amesema serikali imeweka mikakati ya usafiri wa dharura, ikiwemo kutuma helikopta kupeleka mtihani kufikia maeneo ambayo hayawezi kupitika kwa urahisi kutokana na hali mbaya ya barabara.
Aidha, Katibu huyo anatarajiwa kuelekea Elgeyo Marakwet kufuatilia maandalizi ya mitihani ya kitaifa na kuhakikisha kuwa shughuli za elimu zinaendelea kwa utulivu licha ya msiba huo mkubwa.
Serikali imetoa wito kwa wazazi na jamii kwa jumla kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama katika juhudi za kuokoa na kusaidia waathiriwa wa janga hilo.
