Askofu mkuu Makumba; Toharani sio jehanamu

Kanisa linapoadhimisha siku ya kuwakumbuka marehemu wote wakristu wametakiwa siku zote kukumbatia sakramenti ya toba kama njia moja ya kujenga uhusiano kati yao na mwenyezi Mungu.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba amesema kuwa ni vyema kwa kila mmoja kuwa na hulka ya kushiriki toba kwa kuwa ndani ya toba hiyo ina malipizi na msamaha ambayo humjali mkristu nafasi ya kupata huruma ya Mungu.

Amesema kuwa kutoshitriki toba ni sawa na kutenda dhambi kwa kusudi ambayo humweka mkristu katika adhabu ya milele isyopata huruma ya Mungu baada ya kuaga dunia akisema kuwa yule asiye na hulka ya kushiriki toba atasalia katika jehananu ikilinganishwa na yule anayeshiriki toba ambaye roho yake itawekwa toharani wakisubiri huruma ya Mungu.

Askofu Makumba amesema kuwa nyoyo za wale wanaombewa kila mwaka katika siku kuu hii ya kumbukumbu ni za wale walio toharani na wala sio jehanamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *