Jimbo katoliki la Kapsabet litaanza kutumia rasmi divai iliyozinduliwa na Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB mwaka ujao.
Askofu wa Jimbo katoliki la Kapsabet John Lelei amesema kuwa divai hiyo mpya itatumika kuanzia mwaka ujao kwa kuwa parokia mbalimbali zingali na kiasi kikubwa ya divai ambayo imekuwa ikitumika hapo awali ametoa wito kwa parokia hizo kuhakikishia kuwa wanatilia maanani matumizi ya divai hiyo mpya kuanzia mwaka ujao.
Hata hivyo askofu Lelei amebaini kuwa tayari parokia mbalimbali jimboni humo zimeanza kutumia divai hiyo mpya akitoa wito kwa yeyote atakaytaka kununua divai hiyo kufuata taratibu zilizowekwa na Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB.
