Kumbukumbu la nane ya Askofu Korir

Jimbo katoliki la Eldoret limeandaa Misa ya kumbukumbu ya nane tangu kufariki kwa askofu Cornelius Korir.

Askofu wa Jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akihubiri katika misa hiyo amemsifu kama mtu aliyesimamia kikamilifu maswala ya amani katika eneo Pana la bonde la kerio akisema kuwa matunda ya juhudi zake tayari zimeanza kuzaa matunda katika bonde hilo.

Ametoa wito wa majadiliano baina ya pande zinazohasimiana ili kutafuta suluhu na hatimaye amani kwa heshima ya askofu Korir.

Askofu Kimengich amehaidi kutekeleza yale ambayo askofu Korir aliazimia kutekeleza jimboni ametaja kubuniwa kwa Jimbo la Kapsabet kama mojawapo ya ruwaza yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *