Mahakama ya Eldoret imeendelea kuisikiza kesi ya dhulma dhidi ya mwanawe gavana wa kaunti ya Turkana Jeremiah Lomorukai baada ya kudaiwa kuvamiwa na wafuasi wa mbunge Turkana South John Ariko.
Akitoa ushaihidi wake mbele ya Hakimu mkuu mwanadamizi Kesse Cherono,nduguye mlalamishi Lavish Lomorukai alieleza mahakama kuwa alimnusuru mwanawe mnamo Aprili 29 2024 alipofika katika eneo la tukio alipompata nduguye akiwa hajielewi baada ya kupewa kichapo Cha mbwa katika kituo.kimoja Cha kibiashara viungani mwa.mji wa Lodwar.
Lavish pia alieleza mahakama kuwa alikata kauli ya kumpeleka nduguye Nimrod Lomorukai hospitalini kutokana na hali aloyokuwa wakati huo na kuhupiga ripoti mara moja kwa polisi kwa kile alisema maisha ya nduguye yalikuwa hatarini.
Washukiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo akiwa na wengine waliachikiwa kwa thamani ya pesa taslimu ya shillingi 150,000 NebatoLokutuni, David Nangiro, Jemostar Akooyen, Bornfestus Nabuin, JosephEkitela, Sammy Ekitelem ak James Abel.
Upande wa mashtaka umepanga mashahidi 20 ,kesi hiyo itaendelea kusikilizwa baina ya Desemba 11 na 12 mwaka huu.
Upande wa mashtaka umepanga mashahidi 20 ,kesi hiyo itaendelea kusikilizwa baina ya Desemba 11 na 12 mwaka huu.