ARCH.MUHATIA;Acheni kushabikia dhambi

Wakristu wameshauriwa kuasi dhambi na kuhakikisha wanaweka maisha yao ya ukristu sawa sawa ili waweze kujikatia tiketi ya kwenda mbingu.

Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muhatia Makumba alisisitiza kwamba wanadamu kwa sasa wanaonekana kushabikia sana dhambi swala analosema ukristu hudondokea hali hiyo na kuwataka katu kutokubali kurudishwa katika maisha yasiyofaa.

Aidha,askofu mkuu Muhatia alisisitiza haja ya kila mmoja kufanya swala la muhimu na la msingi sala ili iweze kuwaongoza vyema na kujitenga na dhambi ambayo huleta mauti katika maisha ya binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *