Gavana Kinyanjui; Bado Tunawachunguza walio Hospitalini

watu watatu waliokuwa wamelazwa katika chumba cha kipekee  katika hospitali ya nakuru level 5 kuhusiana na virusi vya corona wanaendelea kupokea matibabu huku wawili kati yao wakithibitishwa kuwa hawana virusi hivyo.

 haya kwa mjibu wa gavana wa kaunti hiyo ya nakuru lee kinyanjui akieleza kuwa wameweka mipango  na wahudumu wa hoteli za kifahari pamoja na makanisa kuhakikisha hakuna mkurupuko ambao utashuhudiwa katika kaunti hiyo.

gavana huyo amesema kuwa bada ya ya kufanyiwa uchunguzi wa kinqa na maafisa wa afya wawili walipatikana hawana huku mwingine wa tatu akifanyiwa uchunguzi wa kina.

 amewataka wananchi kutohudhuria mikutano ya hadhara ili kuepukana na maabukizi vya virusi hivyo hatari huku akisema kuwa serikali ya kaunti yaimetoa hamasisho kwa wakaazi na anaamini ya kwamba kaunti yahaitaathiri na virusi hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *