wenyeji katika bonde la Kerio wakiendelea kujikwamua kutoka kwa lindi la utovu wa usalama ambao matunda yake yanaoenekana kadri muda unavyokwenda,askofu wa kanisa la AIC kaunti ya Elgeyo-Marakwet David Kipsoi ameshauri serikali kuhakikisha kwamba wanawahusisha viongozi wa kidini kikamilifu katika upatikanaji wa amani.
akiongea wakati wa maombi ya kila mwaka katika eneo la Kapsait ambayo ni ipo mipakani mwa kaunti za Kerio,askofu huyo alisema kwamba amani haiji iwapo mwenye kuhubiriwa amani hiyo hana imani ya kuhubiriwa swala hilo,huku akiwataka wakazi kuwa tayari kukumbatia mwito huo.
Askofu Kipsoi Vilevile alidokeza kwamba kunyangawa kwa silaha sio suluhu tu ila yapasa serikali kuwa makini na vikundi mbalimbali katika jamii na kufahamu kile wanahitaji.
Askofu huyo kadhalika,aliwataka wenyeji kutambua kwamba iwapo amani haipo hawataweza kuendelea na shughuli zao za kila muda na kuwataka kuwa mabalozi wa amani kila muda.