Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameongoza wakristu katika misa ya ishirini na sita ya amani katika eneo la Kapsait ambayo ni mpaka I pa kaunti ya Elgeiyo Marakwet na Pokot Magharibi.
Akihubiri katika Misa hiyo askofu Kimengich ametoa wito kwa Kila mmoja kudumisha amani akisema kuwa amani hiyo ndio tunu msingi ya umoja wa jamii bila kuangalia Tabaka kabila au cheo.
Amepongeza viongozi waliotangulia katika juhudi za kuleta amani katika eneo Hilo akimtaja askofu mwendazake Cornelius Korir katika juhudi zake za kujisadaka ili kuona kuwa amani inashuhudiwa katika eneo Hilo.
Askofu Kimengich amesema kuwa ukosefu wa usalama ambao umekuwa ukishuhudiwa katika eneo Hilo limerejesha eneo Hilo nyuma kimaendeleo akitoa wito wa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi ili kurejesha Hali ya utulivu.
