Ipo haja ya kuwa na ushrikiano baina mapadre na wakristu katika parokia mbalimbali kama njia moja ya kupiga jeki shughuli za uinjilishaji.
Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima akihubiri katika misa ya daraja la upadre na ushemasi katika uwanja wa shule ya wavulana ya Kibabii jimbo katoliki la Bungoma askofu huyo ametoa wito wa ushirikiano katika parokia mbalimbali baina ya mapadre na wakristu akisema kuwa kule kushikana mikono ndio utakaorahisisha shughuli za uinjilishaji.
Askofu Kadima kadhalika aliwataka mapadre hao wapya kulenga shabaha la kuwaelekeza wakristu katika ramani ya mbinguni akisema kuwa wito huo una changamoto si haba ila kujitolea kwao katika wito huo pamoja na sala ndio mambo msingi yatakayowaongoza katika wito huo.
Amewatahadharisha wakristu dhidi ya kuchochea na kutoa semi za chuki na fitina dhidi ya mapadre kukoma akisema kuwa hulka hiyo sio ukristu na kadhalika italemaza zoezi nzima ya uinjilishaji.