Wakristu wametakiwa kuwa na umoja kwa Kila jambo wanalotekeleza kama njia moja ya kupiga jeki uinjilishaji.
Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich akihubiri katika Misa ya kusherehekea siku ya familia ya parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu kathedrali askofu Kimengich amewahimiza kujitolea kikamilifu katika miradi mbalimbali ya kanisa ambayo anasema itaimarisha umoja jimboni.
Askofu kadhalika aliwaonya wakristu dhidi ya kunung’unika wanapotakiwa kujitolea akiwahimiza kujitolea kikamilifu kwa Upendo na moyo wa ukarimu kama kueneza uinjilishaji.
Alitoa wito kwa Kila moja kujisadaka kwake mwenyezi Mungu kwa kusalimisha udahifu wao kwake akisema kuwa ni kupitia hayo ndipo mja hupata karama.