Mswada wa kifedha wa mwaka wa 2024- 2025 unazidi kupokea upinzani mkali miongoni mwa viongozi wa kidini.
wa hivi punde ni askofu mstaafu wa jimbo katoliki la Kitale Maurice Anthony Crowley ambaye ametoa wito kwa rais William Ruto kuingilia katika akisema kuwa baadhi ya mapendekezo katika mswada huo yananuia kukandamiza mwananchi wa kawaida.
Askofu Crowley kadhalika alisikitia ajali mbaya
za barabarani zinazoshuhudiwa nchini akitoa wito kwa madereva kuwa waangalifu kama njia moja ya kujiepusha ajali hizo.
Kauli yake askofu Crwoley yanajiri siku chahce baada naye askofu mkuu wa kiangilikana nchini Jackson Ole Sapit akiwasilisha mapendekezo yake kuhusiana na swala hilo kwenye bunge la kitaifa,kuwataka wabunge kuhakikisha mswada huo unatupiliwa mbali akisema inawakandamiza wakenya.