TSC haiwezi kutuuzia uwoga

Walimu wa kitengo cha sekondari msingi Junior Secondary ukanda wa North Rift wameapa kuendelea kuandamana hadi pale tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC kusikiza kilio chao na kuafikia matakwa yao.

wakizungumza mjini Eldoret waliposhiriki maandamano ya amani,walimu hao sasa wanasema hawatatishwa na vitisho barisi kutoka kwa TSC na badala yake,watasusia kazi hadi waajiriwe kwa masharti ya kudumu.

yanajiri haya huku walimu hao wa JSS wakishikilia kuwa wanapaswa kuajiriwa kwa masharti ya kudumu kwani wao waliweza kusoma na wanazo vyeti hitajika kuwa waajiri wa tsc.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *