suluhu sio lawama

Askofu wa jimbo la Eldoret Dominic Kimengich amekariri kuwa kuwafukuza na kuwalaumu walimu sio suluhu dhidi ya matokeo duni wa mtihani wa kitaifa ila inawapasa washikadau kwenye sekta ya Elimu kushirikiana.

Akizungumza katika shule ya upili ya wasichana ya  St.Agatha Mokwo wakati wa hafla ya sikukuu na maombi ya shukrani, askofu Kimengich alikashifu hulka hiyo ya kuwanyosheana kidole cha  lawama na kuwavuruga walimu pindi tu  matokeo duni inasajiliwa shuleni.

Aidha askofu Kimengich alisema yawapasa wanafunzi, walimu pamoja na wazazi kushirikiana  ili kufanikisha matokeo bora katika mtihani wa kitaifa. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *