Shirika la kulinda ndege aina ya Korongo nchini la Crane Foundation limesema kwamba limeanza mchakato wa kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwalinda ndege hao walio kwenye hatari ya kusahaulika.
akizungumza katika chuo kikuu cha Eldoret Afisa msimamizi wa shirika la Crane Foundation Dkt.Wanyoiko Wamite ni kwamba waliweka mikakati za kudumu kwa kuwatuma maafisa wake nyanjani ili kuwapa mafundisho ya kutosha wakaazi ili kujiepusha na maswala yanayoweza kuwa chanzo cha kupotea kwa ndege hao kwa nanma wanavyoishi na kutangamana na viumbe hivyo.
Kwa upande wake Richard Kering ambaye ni afisa wa mamlaka ya mazingira NEMA alisisitiza haja ya kushirikiana kati ya wananchi na maafisa wa mazingira kando na washikadau wengine wanaochangia kuimarishwa kwa hewa safi na kupunguza uharibifu na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakati huo Kering alisema serikali ya kitaifa inastahili kuongeza mgao kwenye mamlaka ya NEMA kusaidia kupingana na mabadiliko ya tabi nchi inayochangia kupotea kwa ndege aina ya Korongo.
Ikumbukwe kuwa kaunti ya Uasin Gishu ina ndege wengi wa aina ya Korongo ikiwa ni asilimia 22 ya kitaifa.