Ni afueni kwa wakulima wa kahawa kwenye kaunti hii ya Uasin gishu baada ya wizara ya vyama vya ushirikia na biashara ndogo kupanua soko la zao hilo.
Katika mkutano na wakulima wa kahawa kwenye kaunti hii ya uasin Gishu waziri wa vyama vya ushirika na biashara ndogo Samson Chelugui alitoa wito kwa wakulima kujiunga na vyama vya ushirika na mikopo kamanjia moja ya kunufaika na mpango wa serikali wa kupanua soko la zao hilo.
Waziri huyo alihaidi kuwekeza katika sekta hiyo ili kuwainua wakulima kimaendelea kwa kuwapa mikopo ya kuimarisha ukuzaji na uzalishaji wa zao hilo hapa nchini.
Naye gavana wa kaunti hii ya Uasin gishu Jonathan Bii Chelilim aliwataka wakulima hao kukumbatia kilimo mseto akisema kuwa hii ndio njia moja itakayowafaidi wakulima wa kaunti hii.
Nao wakulima wa zao hilo kwenye kaunti hii walisema kuwa mpango huo wa serikali itawafaidi kwani watapata soko la kuuza mazao yao.