Uasin Gishu; Hofu kwa wakulima nzige wakitua

Wakulima wa zao la parachichi katika eneo Kapseret kaunti ya Uasingishu wameingiwa na hofu baada ya mashamba yao kuvamiwa na nzige.

Nzige hao wameripotiwa kuonekana katika mtaa wa Langas wakti waziri wa kilimo Peter Munya, alipokuwa kwenye hafla ya kufungua maonyesho ya kilimo ambayo yanatarajiwa kukamilika mnamo hii leo.

Nzige hao waliripotiwa kuoneka kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu katika eneo bunge la Moiben, kabla ya kusambaa katika maeneo ya Soy na Kapseret hatua iliopelekea waziri wa kilimo kwenye kaunti hii Silas Yego na mbunge wa Moiben Silas Tiren kuitaka serikali kuu kuchukua upesi hatua za dharura.

Yakijri hayo wenyeji kwenye kaunti ya Transnzoia eneo bunge la Saboti eneo la Kapretwa vilevile wameelezea wasiwasi wao baada ya mashamba yao ya majani chai na kahawa kuvamia na nzige.

Kwa sasa wamelalamikia kuwasili kwa nzige hao katika eneo hilo huenda ukapelekea wao kukosa ajira na mapato kutokana na kilimo hicho.  

Aidha kulingana naye chifu wa Saboti Wechuli Protus ameitaka serikali ya gavana Khaemba kuweka mikakati ya haraka kuokoa sekta hio ya kilimo kwenye kaunti hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *