Ipo haja ya kina mama kuhamasishwa kikamilifu kuhusiana na umuhimu wa kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani na wasiwe chanzo cha vurugu katika jamii.
Kulinganana mwakilishi wa kina mama katika muungano wa kina mama wa amani kaunti ya Uasin Gishu Mary Njogu ni kwamba kina mama wengi vijijini hawajapata ufahamu wa kutosha kusaidia taifa katika upatikanaji wa amani au hata kutoa suluhu la kudumu.
Akiongea wakati wa mkutano wa amani uliondaliwa na muungano wa makanisa NCCK ukanda wa North Rift,Njogu amesema kwamba kwa sasa wakati imebadilika na inawapasa kina mama kuwa mstari wa mbele kusimama na jamii na kuwa mabalozi wa amani.
Amesema kwamba kwa sasa wamebuni sera za kusaidia kina mama mashinani kupata ufahamu kamili kuhusiana na maswala tata ambayo huenda yakawa vyanzo kuu vya vurugu sio tu katika familia bali hata katika taifa.
Aidha,amewataka kina mama kuwa kipaumbele kujitokeza kwa uongozi ndipo waweze kusaidia katika kubadilisha jamii kwa njia inayostahili.
Wakati huo baadhi ya washikadau kutoka mashirika mbalimbali wakiongozwa na mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu mjini Eldoret Nick Omito amebaini kwamba kama washikadau wamehusishwa na mahakama za humu nchini ili kufikisha ujumbe wa kusuluhisha mizozo katika jamii kwa kuwatumia kina mama na namna matumizi ya mfumo mbadala wa kutatua mizozo AJS unaeleweka na kusaidia kutatua utata katika jamii ikiwemo swala la upatikanaji wa amani.
Omite amesema kwamba kwa sasa wanalenga kuweka mipango ya kudumu kwa jamii kuelewa fika swala na kuishi kwa amani ni la umuhimu na utata upi na unaweza kutatuliwa nje ya mahakama.