Serikali yaweka wazi kuwa itanunua mahindi zaidi ya millioni 44 msimu huu

Katibu katika wizara ya kilimo ,mifugo na utunzaji wa mimea nchini Kello Harsame amewahakikishia wakulima kwamba serikali itachukua mahindi yao yote pindi msimu wa mavuno utakapo wadia akisema mikakati ya kutosha imewekwa.

Akizungumza alipozuru bodi ya nafaka na mazao NCBP ya Eldoret katibu huyo alisema kwamba kwa sasa wizara inatarajia kupokea zaidi ya magunia million 44 ya mahindi hii ikiwa ni zaidi ya tani millioni moja ambapo ameweka bayana kwamba serikali iko tayari kupokea mazao hayo.

Vilevile,katibu huyo aliwataka wakulima kuwa waangalifu wasije wakayauza ovyo mahindi yao kwa wafanyibiashara walaghai akisema kwamba serikali inapanga kuwanunulia mazao yao kwa bei nzuri.

Wakati huo aliwataka wakulima kuhakikisha kwamba wanayapeleka mahindi yao kwenye maghala ya kitaifa kukaushwa wajiepushe na hasara akieleza kwamba hadi wa sasa mashine za kukausha mazao yao imekwisha karabatiwa serikali ikilenga kuongeza mashine mengine zaidi ya 10 kwa kila eneo.

Aidha aliweka bayana kwamba serikali haitaagiza mahindi kutoka mataifa za nje ila uagizaji wa mahindi ya rangi ya njano inazingatiwa kupunguza watu kungangania mahindi nyeupe na wanyama na pia kuongeza kapu la taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *