Himizio limetolewa kwa wakristu kuwa na msingi bora wa imani katika familia ili kufanikisha kizazi kijacho kilicho na mwelekeo bora.
Akizungumza wakati wa hafla ya Family day katika parokia Ya Mtakatifu Mikaeli Otiende askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Subira Anyolo amesisitiza haja ya wakristu kusimama imara katika imani yao ili kuwasaidia wanao kuwa wakutegemea katika maisha siku za baadae.
Askofu mkuu vilevile amesikitikia hali ambayo kizazi cha sasa kimeegemea mbinu za kisasa kuzikuza familia zao akisema haistahili akisema kwamba wanapaswa kurejea kwa hulka na mafundisho za kiafrika na kukumbatia tamaduni za familia.
Aidha,amewaomba vijana kujiepusha na utumizi wa mihadarati maana amesema itawaelekeza pabaya katika maisha ya baadae.