Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim amepuuzilia mbali matokeo ya utafiti ulioorodhesha serikali yake kuwa ya mwisho katika utendakazi nchini.
Kulingana na utafiti uliofanywa na kampuni moja ya utafiti ISS Africa – Kenya kwa ushirikiano na City Hub Limited, kati ya tarehe 24 – 26 August, mwaka huu iliorodhesha kaunti hii ya uasin gishu kuwa nambari arobaini na saba kati ya kaunti zote arobaini na saba.
Gavana bii amepuzilia mbali utafiti huo akisema kuwa matokeo hayo yalifadhiliwa na maasidi wake kisiasa akipongeza mkaguzi wa hesabu za serikali kubainisha Uasin Gishu ni miongoni mwa kaunti ambazo zilitumia fedha zao, uasingishu ikitumia asilimia 71.3 kwa fedha zilizotengewa maendeleo.
Kadhalika amewataka wapinzani wake kumuunga mkono katika juhudi zake za kutekeleze miradi ya maendeleo yanayonogeshwa kwenye nguzo yake kumi ya maendeleo aliyohaidi wakaazi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.