Wanafunzi 22 Wapepea ElgeiyoMarakwet

Serikali ya kaunti ya Elgeyo Marakwet imezindua kundi la wanafunzi 22 ambao watasafiri kuelekea nchini Australia kuendeleza masomo yao kupitia mradi kwa jina PEPEA ulioanzishwa na gavana wa kaunti hiyo Wesley Rotich.

Kulingana na gavana Rotich, mradi huo umekuwa wa mafanikio kwa wakazi wa kaunti hiyo ambao wana nia ya kusafiri nchi za nje kuongeza masoma yao.

Hafla hiyo ilifanyika mjini Iten huku serikali ya kaunti ikikiri kupitia changomoto kutafuta vyuo vikuu katika nchi za ng’ambo vyenye kiwango chini cha karo.

Waliofaidika na mpango huo ni wanafunzi 22 ambao walilipa shilingi 600,000 kila mmoja.

Gavana Rotich aidha, amedokeza kuwa mradi huo wa PEPEA utatoa fursa kwa vijana kwenye kaunti ya Elgeyo Marakwet kuzuru nchi za nje kuendeleza masomo ili kuboresha maisha yao ya halafu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *