Askofu mkuu wa kanisa la Kiangilakana nchini Jackson Ole Sapit amiwataka wakenya na viongozi wote kuhakikisha wanatatua migogoro miongoni mwao kwa njia ya amani.
Akizungumza katika kanisa la St.Stephen Cathedral jijini Nairobi amesikitia hali ambayo kila kukicha kunashuhudiwa visa visivyostahili watu wanapokosa kuafikiana kwa hili akisema sharti ikome na njia mwafaka na ya amani ifuatiliwe kikamilifu.
Afskofu huyo vilevile amewataka wakenya kutambua kwamba taifa hili pindi inapovurugwa shughuli a juhudi za kuinua uchumi wan chi huathirika pakubwa na hivyo kuwataka kuwa makini na maamuzi yao
Wakati huo,Ole sapit amewataka wakristu kuwa na mwelekeo uliobora ya kiimani kwa kuwa wakristu waaminifu katika kristu akiwapa motisha kwamba kila muda ulimwengu unabuni maswala mengi na tofauti ambayo amesema iwapo hawatakuwa makini nazo watatumbukia katika kaburi ya mauti na imani yao kuzamishwa.