Manaibu kwa uwazi

Muungano wa wahadhiri kaunti ya Uasin Gishu UASU umetoa wito kwa wizara ya elimu nchini kukoma kuwateua manaibu chansela kwa misingi ya kikabila bali waangalie tajiriba aliyo nayo mwadhiri.

Wakizungumza mjini Eldoret,wakiongozwa na katibu wa muungano huo Philip Chebunet alisema kwamba wahadhiri wanayouwezo mkubwa wa kuliongoza chuo na iwapo kutakuwepo na mbinu usiostahili ukitumika utachangia pakubwa kwa vyuo vingi kukosa kuendelea vyema kwa shughuli zake.

Wamesema kwamba hatua maalum isipozingatiwa huenda maswala ya kupambana na ufisadi usiafikiwe na hivyo kuitaka wizara kuwa makini na maamuzi yake.

Wakati huo,muungano huo ulitoa pendekezo kwa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC kuwachunguza manaibu chansela kabla ya kuwaingiza wengine ofisi ndipo mali ya shule iweze kulindwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *