Takriban watu elfu kumi wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la ugatuzi mwaka huu litakalofanyika katika kaunti hii ya Uasin Gishu.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati andalizi Ahmed Abdulahi tayari watu elfu nne wamejiandikisha ikiwa ni takriban wiki mbili tu kabla ya kongamano lenyewe kufanyika, Ahmed ameyasema hayo baada ya mkutano uliowahusisha viongozi wa kaunti katibu wa ugatuzi na uwakilishi wa baraza la magavana na bunge la kaunti ya uasin gishu katika harakati za mwisho mwisho.