Mahakama yahalalisha mswada wa fedha 2023

Mahakama ya Rufaa imebatilisha agizo lililokuwa limetolewa na mahakama kuu ya kuzuia utelezwaji wa sheria ya fedha ya mwaka wa 2023 hadi rufaa iliyowasilishwa na serikali itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Kwa mujibu wa uamuzi wa  majaji Mohamed Warsame Hellen Omondi na Kathurima inoti mahakama kuu ilikosea kwa kusitisha utekelezaji wa sheria hiyo badala ya kusitisha vipengele vyenye utata, wakisema kuwa kusitishwa kwa sheria hiyo, kulikwenda kinyume na hitaji la kuangalia athari zake kwa umma yaani public interest. 

Sheria hiyo tata ya fedha ya mwaka 2023 ilisitishwa na jaji Mugure Thambi, kufuatia kesi iliyowasilishwa na seneta wa kaunti ya Busia Okiya Omtata na wengine sita wakipinga mchakato mzima wa kubuni sheria hiyo na vile vile kukosoa baadhi ya vipengele.

Baada ya uamuzi wa kusitisha utekelezaji kudumishwa tarehe kumi mwezi huu, serikali kupitia mwanasheria mkuu wa serikali  Justin Muturi iliwasilisha rufaa hiyo, haya yanajiri huku majaji watatu wakiteuliwa kusikiliza wakiwemo David Majanja, Lawrence Mugambi na  Christine Miole.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *