padre Charles Kirui aliwataka wakristu kujifunza sala ya shukrani badala ya sala ya kunung’unika kila wakati.
akihubiri katika misa ya sherehe ya Mtakatifu Anna na Joachim padre Kirui alisema kuwa shukrani kwa mwenyezi Mungu huzaa baraka na neema tele kwa kila mkristu.
amewahimiza wakristo kutambua kuwa njia pekee ya kuupata ufalme wa mbinguni ni kulisifu neno lake kando na changamoto wanazopitia.