Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kupitia wizara ya biashara na viwanda ilitoa zaidi ya shillingi millioni 650 ambazo zilitolewa kwa vyama vya ushirika 178 katika kaunti ya Uasin Gishu kusaidia katika ukuaji wa vyama hivyo.
Kwa mujibu wa gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim ni kwamba kupitia mashirika hayo wakulima na wafanyibiashara mbalimbali kwenye vikundi hivyo wameweza kupanua biashara na mapato yao huku akiongeza yastahili wanaanchi kujiunga na vyama hivyo kama njia moja ya kuendelea katika maisha na kupunguza umaskini.
Gavana huyo alitaja umuhimu wa kila mkaazi kujihusisha na vyama vya ushirika na mikopo ndipo waweze pia kubadilisha maisha yao akieleza kwamba wengi wa wanachama wameweza kujisimamia kimaisha kutokana na kile wanapokea kwenye vyama vyao.